İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
Sure 5

Al-Maaida

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 54

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِۦ فَسَوْفَ يَأْتِى ٱللَّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُۥٓ أَذِلَّةٍ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ يُجَـٰهِدُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَآئِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ ٱللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ 54

{54} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba Yeye ndiye asiyewahitaji walimwengu. Na kwamba mwenye kuiacha dini yake, basi hatamdhuru Mwenyezi Mungu chochote, bali anajidhuru mwenyewe. Na kwamba Mwenyezi Mungu anao waja wanaompwekesha Yeye, na wanaume wakweli, ambao Yeye Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu alichukua dhamana ya kuwaongoa na akaahidi kuwaleta. Na kwamba wao ndio wakamilifu zaidi wa viumbe wote katika sifa na wenye nguvu wao zaidi katika nafsi, na wazuri zaidi katika tabia. Sifa yao kubwa zaidi ni kwamba Mwenyezi Mungu "anawapenda nao wanampenda." Kwa sababu Upendo wa Mwenyezi Mungu kwa mja ndiyo neema kubwa zaidi aliyopewa na fadhila bora zaidi aliyopewa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anapompenda mja, anamsahilishia njia, na anamrahisishia kila gumu, na anamwezesha kutenda mema na kuacha maovu, na anazielekeza nyoyo za waja wake kwake kwa mapenzi. Na katika matakwa ya mapenzi ya mja kwa Mola wake Mlezi ni kuwa, ni lazima awe na sifa ya kumfuata Mtume – rehema na amani ziwe juu yake – kwa nje na ndani katika maneno yake, na vitendo vyake, na hali zake zote. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atawapenda." Kama vile pia katika matakwa ya upendo wa Mwenyezi Mungu kwa mja ni kwamba mja ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu kwa wingi wa mambo ya faradhi na ya sunnah. Kama alivyosema Mtume - rehema na Amani zimshukie - katika Hadithi sahihi kutoka kwa Mwenyezi Mungu: “Na Mja wangu hatanikurubia kwa kitu nikipendacho zaidi kuliko kile nilichomwajibishia. Na mja wangu hataacha kuendelea kujikurubisha kwangu kwa matendo ya sunnah mpaka nimpende. Na nikimpenda, ninakuwa sikio lake analosikia kwalo, na macho yake anayoona kwayo, na mkono wake anaokamata kwao, na mguu wake anaotembea kwao. Na akiniuliza, nitampa. Na akiomba kujikinga kwangu, ninampa kinga.” Na katika matakwa ya kumpenda Mwenyezi Mungu ni kumjua Yeye, mtukufu na kumkumbuka kwa wingi. Kwa sababu Upendo bila ya kuwa ana elimu kumhusu Mwenyezi Mungu ni mapungufu sana, bali hata haupo, hata kama madai ya hilo yatapatikana. Na mwenye kumpenda Mwenyezi Mungu, anazidisha kumkumbuka. Na Mwenyezi Mungu anapompenda mja, anakubali kiasi kidogo cha matendo kutoka kwake, na anamfutia mengi ya makosa yake. Na Miongoni mwa sifa zao ni kuwa, ni "wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri." Wao kwa Waumini ni wanyenyekevu kwa sababu ya mapenzi yao kwao, nasaha zao kwao, na ulaini wao, na upole wao, na huruma yao kwao, na rehema yao kwao, na urahisi kuamiliana kwao, na ukaribu wa jambo linalotakiwa kwao, nao ni wenye nguvu juu ya makafiri waliomkufuru Mwenyezi Mungu, wanaofanyia ukaidi aya zake, wanaokadhibisha Mitume wake. Hima zao na maazimio yao yaliungana juu ya kuwapinga, na wakafanya juhudi zao katika kila njia ambayo kwayo kupata ushindi juu yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Basi waandalieni muwezavyo katika nguvu, na kwa farasi waliofungwa tayari, ili muwatishie kwa hayo maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu." Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao." "Basi ukali mkubwa dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu ni katika yale yanayomkurubisha mja kwa Mwenyezi Mungu, na mja anaafikiana na Mola wake Mlezi katika hasira yake dhidi yao. Na ukali juu yao na ugumu havizuii kuwalingania kwenye Dini ya Kiislamu kwa njia iliyo nzuri zaidi. Kwa hivyo vinaunganishwa ukali juu yao na ulaini katika kuwalingania, na mambo mawili haya yote ni kwa maslahi yao, na manufaa yake yanarejea kwao. "Wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu" kwa mali zao na nafsi zao, na kwa kauli zao na vitendo vyao. "Wala hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu," bali wanaitanguliza radhi ya Mola wao Mlezi na hofu ya lawama yake kuliko lawama za viumbe. Na hili linaashiria nguvu ya hima zao na maazimio yao. Kwa sababu mwenye moyo dhaifu, mwenye azimio dhaifu, azimio lake huvunjika wakati anapolaumiwa na wenye kulaumu, na nguvu zake hupungua wakati anapodhalilishwa na wenye kudhalilisha. Na katika mioyo yao kuna kumuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu,kulingana na yale yaloyomo ya kuwaangalia viumbe, na kutanguliza ridha yao na lawama yao mbele ya jambo la Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo Moyo hauwi salama kutokana na kumwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu mpaka usiogope kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama ya yeyote mwenye kulaumu. Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowasifu kwa sifa nzuri alizowaneemesha kwazo, na fadhila za hali ya juu ambazo linalazimu yale ambayo hayakutajwa miongoni mwa mambo mema, akajulisha kwamba hayo ni katika fadhila yake juu yao na wema wake. Ili wasijione na nafsi zao, na ili wamshukuru yule aliyewaneemesha kwa hayo; Ili awazidishie katika fadhila zake, na ili wengine wajue kwamba fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hazina kizuizi chochote. Kwa hivyo akasema, "Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua vyema." Yaani, ni mwenye wasaa wa fadhila na wema, mwenye kupeana kwa mwingi, ambaye rehema yake imeenea kila kitu, na anawakunjulia marafiki zake katika fadhila Zake kitu ambacho hakiwi kwa wasiokuwa hao, lakini Yeye ni Mwenye elimu kuhusu anayestahiki fadhila, ili ampe. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni wapi anaweka ujumbe wake, shina na matawi (yani mitume wenyewe na wale wanaofikisha ujumbe kutoka kwao).