Al-Maaida
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ٱبْنَىْ ءَادَمَ بِٱلْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ ٱلْـَٔاخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلْمُتَّقِينَ 27
{27} Yani wasimulie watu na uwaambie kisa hicho ambacho kilitokea kwa wana wawili wa Adam kwa haki, kisomo ambacho wanaokizingatia watakizingatia kuwa ni ukweli, sio uongo, wala mchezo. Na maana ya dhahiri ni kwamba wana hao wawili wa Adamu ni wanawe wa kutoka mgongoni kwake kama inavyoonyeshwa na maana dhahiri ya Aya na muktadha wake. Na hii ndiyo kauli ya wengi wa wafasiri. Yaani, wasomee habari yao wawili katika hali waliyotoa dhabihu ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, ambayo iliwapelekea kwenye hali iliyotajwa. "Walipotoa mhanga," Yaani, kila mmoja wao alitoa kitu katika mali yake kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, "basi ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwingine haukukubaliwa." Kwa kujua hilo kupitia habari kutoka mbinguni au kupitia kwa desturi iliyotangulia miongoni mwa umma kwamba, alama ya Mwenyezi Mungu kukubali mhanga ni kwamba moto ushuke kutoka mbinguni na uuteketeze. "Akasema" yule mwana ambaye haukupokewa kutoka kwake akimwambia mwenziwe kwa husuda na dhuluma, "lazima nitakuua," naye huyo mwingine akamwambia kwa upole katika hilo. "Hakika Mwenyezi Mungu hupokea tu kutoka kwa wachamungu." Ni dhambi gani au kosa langu gani lililokufanya uniue isipokuwa nilimcha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambaye kumcha Yeye ni wajibu kwangu, na kwako na kwa kila mmoja? Na kauli iliyo sahihi zaidi katika kutafsiri {mchamungu} hapa ni wenye kumcha Mwenyezi Mungu katika matendo hayo; kwa namna kwamba yawe matendo yao ni kwa kuukusudia uso wa Mwenyezi Mungu tu. Na kwa kufuata ndani yake Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake.