Al-Maaida
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ يَـٰقَوْمِ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنۢبِيَآءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكًا وَءَاتَىٰكُم مَّا لَمْ يُؤْتِ أَحَدًا مِّنَ ٱلْعَـٰلَمِينَ 20
{20} Mwenyezi Mungu alipomneemesha Musa na watu wake kwa kuwaokoa kutoka kwa Firauni na kaumu wake na kuwafanya kwao mateka na kuwakandamiza, wakaenda huku wamekusudia nchi zao na makazi yao, nayo ni Bayt al-Maqdis na viunga vyake. Na walikuwa karibu kufika Bayt al-Maqdis, na Mwenyezi Mungu alikuwa amewaandikia jihadi dhidi ya adui wao ili wamfukuze kutoka katika makazi yao. Basi Musa amani iwe juu yake, akawaidhi na akawakumbusha waende katika jihadi. Kwa hivyo akasema, "Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu," kwa nyoyo zenu na ndimi zenu. Kwa maana kuzikumbuka inaita katika kumpenda Yeye Mtukufu na yenye kumtia mtu nguvu juu ya ibada. "Alipowateua Manabii kati yenu," wanaowalingania kwenye uwongofu, kuwaonya kutokana na kuangamia, na wanawahimiza kwenye furaha yenu ya milele, na wanawafundisha yale ambayo hamkuwa mnayajua. "Na akawafanya wamiliki," wenye kumiliki mambo yenu, kwa sababu mmeondokewa na kukandamizwa kwa adui yenu, basi mkawa mnamiliki mambo yenu, na mkaweza kusimamisha Dini yenu. "Na akawapa," katika neema ya kidini na ya kidunia "yale ambayo hakuwapa wowote katika walimwengu." Kwani wao wakati huo walikuwa viumbe bora zaidi na watukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Na akawaneemesha kwa neema ambazo hawakupewa wasiokuwa wao. Kwa hivyo akawakumbusha neema za kidini na za kidunia kitu ambacho kinaitia kuamini kwao na uthabiti wake na uthabiti wao katika jihadi na kuiendea.