Al-Maaida
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَن يَبْسُطُوٓا۟ إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ 11
{11} Yeye Mtukufu anawakumbusha waja Wake Waumini juu ya neema zake kubwa, na anawahimiza juu ya kuzikumbuka kwa moyo na ulimi. Na kwamba kama vile wanavyoona kuwa kuwaua kwao maadui zao, na kuchukua mali zao na nchi zao, na kuwateka kwamba ni neema, basi na waone pia neema yake juu yao ya kuizuia mikono ya maadui wao dhidi yao; na kurudisha vitimbi vyao katika shingo zao kwamba ni neema. Kwani wao ni maadui ambao wametaka jambo fulani, na wakadhani kwamba wana uwezo juu yake. Kwa hivyo ikiwa hawatafikia malengo yao kwa Waumini, basi hiyo ni nusura kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake Waumini. Inawapasa wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hayo, na wamwabudu, na wamkumbuke. Na Haya yanajumuisha kila mwenye kutaka kuwadhuru Waumini, kama vile kafiri, na mnafiki, na mwenye kupindukia mipaka, Mwenyezi Mungu aliwazuia Waislamu shari yao; basi yeye anaingia katika aya hii. Kisha akawaamrisha yale wanayoweza kutafuta msaada kwa yale ambayo wanaweza kujisaidia kwayo katika kuwashinda adui zao na katika mambo yao yote,. Akasema, "Na kwa Mwenyezi Mungu, basi na wategemee Waumini." Yaani, wamtegemee Yeye katika kuleta masilahi yao ya kidini na ya kidunia, na wajitenge na hila zao wala nguvu zao, na wawe na imani na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kufikia yale wanayoyapenda. Na kulingana na imani ya mja kunakuwa kutegemea kwake, na hilo ni katika majukumu ya moyo yaliyokubaliwa juu yake.