İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Jaathiya
Sure 45

Al-Jaathiya

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

6–10. âyetler

تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِٱلْحَقِّ ۖ فَبِأَىِّ حَدِيثٍۭ بَعْدَ ٱللَّهِ وَءَايَـٰتِهِۦ يُؤْمِنُونَ 6 وَيْلٌ لِّكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ 7 يَسْمَعُ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ 8 وَإِذَا عَلِمَ مِنْ ءَايَـٰتِنَا شَيْـًٔا ٱتَّخَذَهَا هُزُوًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ 9 مِّن وَرَآئِهِمْ جَهَنَّمُ ۖ وَلَا يُغْنِى عَنْهُم مَّا كَسَبُوا۟ شَيْـًٔا وَلَا مَا ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوْلِيَآءَ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ 10

{6 - 10} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akawagawanya watu kulingana na kunufaika na Ishara zake au la katika makundi mawili. Kundi la watu wanaozitumia kama ushahidi na kuzitafakari, na kunufaika nazo na kuinuka juu. Na hawa ni wanaomwamini Mwenyezi Mungu, Malaika wake, vitabu vyake, Mitume wake, na Siku ya Mwisho kwa imani kamili, ambayo iliwafikisha katika kiwango cha yakini. Kwa hivyo imani hiyo ikawatakasa akili, ikawaongeza maarifa na ufahamu wao na elimu zao. Na kuna kundi ambalo linasikia ishara za Mwenyezi Mungu kusikia kwa kuwasimamishia tu hoja, kisha wanazipa mgongo na kufanya kiburi kana kwamba hawakuzisikia. Kwa sababu hazikuutakasa moyo wake wala kuusafisha. Bali kwa sababu ya kuzifanyia kwake kiburi, akazidi kupotoka, na kwamba anapojua chochote katika Ishara za Mwenyezi Mungu, anazifanyia mzaha, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akamtishia kwa adhabu kali. Akasema: "'Ole wake kila mzushi mwenye dhambi!'" Yaani, mwongo mkubwa katika anayoyasema, mwenye dhambi sana katika vitendo vyake, na akajulisha kuwa atapata adhabu chungu, na kwamba "nyuma yao ipo Jahannamu," ambayo inatosha kuwaadhibu vikali mno, na kwamba "waliyoyachuma hayatawafaa hata kidogo" miongoni mwa mali "wala walinzi waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu." Kwa hivyo, wakawa wamewatupa katika wakati ambao waliwahitaji sana, ikiwa wangeweza kuwanufaisha.