An-Nisaa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
هَـٰٓأَنتُمْ هَـٰٓؤُلَآءِ جَـٰدَلْتُمْ عَنْهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا فَمَن يُجَـٰدِلُ ٱللَّهَ عَنْهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا 109
{109} “Hivi ni nyinyi hawa mnaowatetea hawa katika uhai huu wa duniani. Basi ni nani atakayewatetea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama? Au ni nani atakuwa wakili wao wa kumtegemea?” Yani chukulieni kuwa mliwabishania katika maisha haya ya dunia, kubishana kwenu huko kukawaondolea baadhi ya yale wanayoyaogopa ya aibu na fedheha mbele ya viumbe, lakini ni nini kitawasaidia na kuwanufaisha? Na ni nani atakayewabishania dhidi ya Mwenyezi Mungu Siku ya Qiyama hoja itakapowaelekea, na zikashuhudia dhidi yao ndimi zao, na mikono yao, miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyafanya? Siku hiyo, Mwenyezi Mungu atawapa kikamilifu malipo yao ya haki, na watajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye haki iliyo wazi. Basi ni nani atakayewabishania dhidi ya yule Mwenye kujua siri, na yaliyofichika zaidi, ambaye atawawekea dhidi yao mashahidi ambao haiwezekani kuwakanusha? Na katika Aya hii kuna mwongozo wa kulinganisha baina ya masilahi ya kidunia yanayofikiriwa yanayotokana na kuacha maamrisho ya Mwenyezi Mungu, au kufanya makatazo yake na yale yanayopotea miongoni mwa thawabu ya Akhera au yanayotokea miongoni mwa adhabu zake. Basi aseme yule ambaye nafsi yake imemwamrisha kuachana na amri ya Mwenyezi Mungu: Wewe huyu hapa umeiacha amri yake kwa uvivu na kupuuza. Basi ni manufaa gani ambayo umefaidika kwa hilo? Na ni nini ulichokosa katika thawabu za Akhera? Na ni nini kilichotokana na kuachwa huku cha upotovu, na kunyimwa, na kuambulia patupu, na hasara? Na vile vile nafsi yake ikimwita kwenye yale anayoyataka miongoni mwa matamanio ya haramu, aiambie: Chukulia kwamba ulifanya yale unayotamani. Kwani, starehe yake inaisha, kisha inafuatwa na wasiwasi, na huzuni, na majuto, kukosa thawabu, na kupata adhabu, ambayo baadhi yake inamtosha mwenye akili kujiepusha nayo. Na hili ni miongoni mwa mambo makubwa zaidi yanayomnufaisha mja kuyazingatia, nalo ni sifa maalum ya akili ya kihakika. Tofauti na mwenye kudai kwamba ana akili ilhali hayuko hivyo. Basi yeye kwa ujinga wake na udhalimu wake, anapendelea starehe ya sasa na raha ya sasa, hata kama matokeo yake ni ya namna gani. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuombwa msaada.