Az-Zumar
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
لِيُكَفِّرَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ أَسْوَأَ ٱلَّذِى عَمِلُوا۟ وَيَجْزِيَهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ 35
{35} "Ili Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu waliyoufanya na awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema waliokuwa wakiutenda." Matendo ya mwanadamu ya hali tatu: ima ni mbaya zaidi au bora zaidi au si mbaya zaidi wala bora zaidi. Sehemu hii ya mwisho ndiyo inajumuisha yale yanayoruhusiwa ambayo hayaambatani na malipo wala adhabu. Nayo mabaya zaidi yanajumuisha maasia yote. Nayo mazuri zaidi yanajumuisha mambo yote ya utiifu. Kupitia maelezo haya, maana ya Aya hii inadhihirika, na kwamba kauli yake: "Ili Mwenyezi Mungu awafutie ukomo wa uovu waliyoufanya," yaani, madhambi yao madogo na makubwa kwa sababu ya wema wao na uchamungu wao, "na awalipe ujira wao kwa mujibu wa ukomo wa wema waliokuwa wakiutenda." Kwani, "hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja. Na ikiwa ni jambo jema, basi Yeye hulizidisha na hutoa kutoka kwake malipo makubwa."