Al-Ankaboot
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ 61 ٱللَّهُ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ وَيَقْدِرُ لَهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ 62 وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَحْيَا بِهِ ٱلْأَرْضَ مِنۢ بَعْدِ مَوْتِهَا لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُ ۚ قُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ 63
{61-63} Huku ni kuwasimamishia hoja washirikina ambao wanakadhibisha upweke wa Mwenyezi Mungu na kwamba Yeye tu ndiye anayefaa kuabudiwa, kwa kuwafanya wakiri hilo kwa kutumia ushahidi wa upweke wake katika umola ambao wao wenyewe wanauthibitisha. Kwani, ikiwa "utawauliza ni nani aliyeumba mbingu na ardhi" Na ni nani aliyeteremsha maji kutoka mbinguni, na akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake? Na ni nani ambaye uendeshaji wa viumbe vyote uko mkononi mwake? "Bila ya shaka watasema: Ni Mwenyezi Mungu" peke yake; na wakakiri kwamba masanamu na hao waliowaabudu pamoja na Mwenyezi Mungu hawawezi chochote katika hayo! Basi unaweza kustaajabia uzushi wao na uongo wao huo, na kumuendea kwao yule waliyekiri kutojiweza kwake na kwamba hastahili kuendesha chochote! Na utatambua kwamba hawana akili, na kwamba wao ndio wapumbavu wenye maono dhaifu! Basi je, unaweza kumuona yule ambaye ni dhaifu zaidi wa akili na maono kuliko mwenye kulijia jiwe au kaburi au mfano wake ilhali anajua kwamba halifai, wala halidhuru, wala haliumbi, wala haliruzuku - kisha akalikusudia hilo tu, na akalifanyia ibada hilo tu ibada, na akalishirikisha pamoja na Mola Mlezi, Muumba, Mwenye kuruzuku, Mwenye kunufaisha, Mwenye kudhuru? Na sema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyebainisha uwongofu na upotofu, na akaweka wazi upotofu ambao washirikina wanafanya ili wale waliofanikiwa wawezi kujitahadhari nao. Na sema: Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyeumba ulimwengu wa juu na wa chini, na akawaendesha na kuwaruzuku huku akimkunjulia riziki hiyo amtakaye, na akamkunjia amtakaye kwa hekima yake, na kwa sababu anajua kile kilicho kizuri kwa waja.