Al-Furqaan
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱسْجُدُوا۟ لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا۟ وَمَا ٱلرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ۩ 60
{60} Na ndiyo maana akasema, "Na wanapoambiwa: Msujudieni Arrahman (Mwingi wa rehema!)" Yaani Yeye peke yake, aliyewaneemesha kwa neema zote, na akawazuilia adhabu zote. "Wao husema" kwa kukataa na kukufuru, "Ni nani Arrahman (Mwingi wa rehema?)" - Kwa madai yao potofu, wanasema kwamba hawamjui Arrahman (Mwingi wa rehema). Na walifanya miongoni mwa mambo wanayomshutumu nayo Mtume, ni kwamba walisema: Anatukataza sisi kuchukua miungu wengine pamoja na Mwenyezi Mungu, ilhali yeye anamuomba pamoja naye mungu mwengine. Anasema: Ewe Arrahman (Mwingi wa rehema) na mfano wa hivyo. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Sema: Mwombeni Mwenyezi Mungu, au mwombeni Rahman (Mwingi wa rehema), kwa jina lolote mnalomwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri." Majina yake Mtukufu ni mengi, kwa sababu ya wingi wa sifa zake na wingi wa ukamilifu wake; kila moja yake linaonyesha sifa ya ukamilifu. "Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe tu?" Na hili ni kwa msingi wa kwamba walimkadhibisha Mtume na wakamfanyia kiburi kumtii. "Na huwazidishia" kuwalingania kwake wamsujudie Mwingi wa rehema, "kujitenga mbali" na haki wakaiendea batili na wakazidisha ukafiri na kuwa mashakani.