Al-Kahf
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَلَبِثُوا۟ فِى كَهْفِهِمْ ثَلَـٰثَ مِا۟ئَةٍ سِنِينَ وَٱزْدَادُوا۟ تِسْعًا 25 قُلِ ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثُوا۟ ۖ لَهُۥ غَيْبُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ أَبْصِرْ بِهِۦ وَأَسْمِعْ ۚ مَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِىٍّ وَلَا يُشْرِكُ فِى حُكْمِهِۦٓ أَحَدًا 26
{25 - 26} Pale Mwenyezi Mungu alipomkataza kuuliza fatwa Watu wa Kitabu juu ya watu wale wa Pangoni kwa sababu hawana elimu yoyote kuhusu hilo, na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi siri na dhahiri, Mwenye kujua kila kitu. Mwenyezi Mungu akamjulisha kuhusu muda waliokaa, na kwamba Yeye peke yake ndiye aliyejua hilo. Kwani hilo ni katika ghaibu ya mbingu na ardhi, na ghaibu yake hiyo ni mahsusi kwake tu. Kwa hivyo, yale aliyojulisha juu yake kupitia ndimi za Mitume wake, basi hayo ndiyo haki ya yakini ambayo haishukiwi. Na yale ambayo hakuwajulisha Mitume wake, basi hakuna yeyote miongoni mwa viumbe anayeyajua. Na kauli yake, "Kuona vyema kulikoje kwake na kusikia kuzuri kulikoje!" Ni mshangao juu ya ukamilifu wa kusikia kwake na kuona kwake, na kuzungukwa kwake yote yanayosikika na yanayoonekana, baada ya kujulisha juu ya kuzungukwa kwa elimu yake mambo yote. Kisha akajulisha kuhusu upekee wake katika ulinzi wa kiujumla na wa mahususi. Basi Yeye ndiye mlinzi ambaye anasimamia uendeshaji wa ulimwengu wote, na ni mlinzi wa waja wake waumini. Anawatoa katika giza mbalimbali hadi katika nuru, na anawasahilishia yawe mepesi, na anawaepusha ugumu. Na ndiyo maana akasema, “Hawana mlinzi yeyote isipokuwa Yeye." Yaani, Yeye ndiye aliyewasimamia wale watu wa pangoni kwa upole wake na ukarimu wake, na wala hakuwakabidhi kwa yeyote katika viumbe. "wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake." Na hii linajumusisha hukumu ya kimajaliwa na hukumu ya kisheria ya kidini. Yeye ndiye anayehukumu katika viumbe wake kwa kutoa hukumu juu ya hatima yao, kuumba na kuendesha, naye ndiye anayewahukumu kwa amri yake, makatazo yake, thawabu zake na adhabu yake. Na alipojulisha kwamba yeye Mtukufu ndiye ana ghaibu ya mbingu na ardhi, kwa hivyo hakuna njia kwa kiumbe yeyote kuifikia isipokuwa kwa njia ile ambayo kwayo anawajulisha waja wake, na pindi Qur-ani hii ilipokuwa ina mengi ya ghaibu, Yeye Mtukufu akawaamrisha watu waikusudie Qur-ani hii, akasema: