İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Israa
Sure 17

Al-Israa

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 33

وَلَا تَقْتُلُوا۟ ٱلنَّفْسَ ٱلَّتِى حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلْحَقِّ ۗ وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِۦ سُلْطَـٰنًا فَلَا يُسْرِف فِّى ٱلْقَتْلِ ۖ إِنَّهُۥ كَانَ مَنصُورًا 33

{33} Na hili linajumuisha kila nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha sawa iwe ni ndogo, kubwa, ya kiume, ya kike, huru, ya mtumwa, ya Mwislamu, na ya kafiri ambaye ana agano ya amani na Waislamu. "Isipokuwa kwa haki" kama vile kuua nafsi kwa sababu nafsi hiyo iliua pia, mzinzi aliyeoleka, mwenye kuiacha dini yake ya Uislamu na akajitenga na kundi la Waislamu, na wale wanaompiga vita kiongozi mkuu katika hali ya vita vyao ikiwa hawawezi kuzuilika isipokuwa kwa kuwaua. "Na aliyeuawa kwa kudhulumiwa." Yaani, bila haki, "basi hakika tumempa mamlaka" yaani hoja iliyo dhahiri ya kufanya kisasi kama vile kuua muuaji, "mrithi wake" naye ni yule aliye karibu zaidi na maiti miongoni mwa warithi wanaochukua mali iliyosalia au warithi wengineo. Na pia tumempa mamlaka ya kimajaaliwa juu ya hilo, wakati masharti ya adhabu ya kisasi yatakapotimizwa, kama vile mauaji ya makusudi, kukiuka mipaka, nafsi mbili hizo kutoshana. "Lakini asipitilize kiasi" mrithi huyo "katika kuua, kwani yeye anasaidiwa." Na kupitiliza kiasi ni kuvuka mipaka, ima kwa kumkatakata anayemuua huyo, au kumuua kwa kile ambacho hakumuua kwacho, au kumuua muuaji halisi. Na katika aya hii, kuna ushahidi kwamba haki ya kuua ni ya mrithi wake, kwa hivyo hairuhusiki kufanya kisasi isipokuwa kwa idhini yake .Na ikiwa atasamehe, basi adhabu ya kisasi hiyo itaanguka, na kwamba mrithi wa aliyeuawa anasaidiwa na Mwenyezi Mungu dhidi ya muuaji na wale waliomsaidia mpaka aweze kumuua naye pia.