Yunus
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَٱتَّبِعْ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيْكَ وَٱصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ ٱللَّهُ ۚ وَهُوَ خَيْرُ ٱلْحَـٰكِمِينَ 109
{109} {Na fuata} Ewe Mtume, yale yaliyoteremshwa kwako kwa matendo na kwa kujifunza, na katika hali zote, na katika kulingania kwayo "{Na vimulia} juu ya hayo. Kwani hii ndiyo aina ya juu zaidi ya uvumilivu, na hakika mwisho wake ni wa kusifiwa. Kwa hivyo usiwe mvivu wala usilalamike. bali dumu juu ya hayo na usimame imara, {mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu} baina yako na yule anayekukadhibisha. {na Yeye ndiye mbora wa mahakimu" Kwa maana hekima yake inajumuisha uadilifu kamili na kufanya haki ambayo unasifiwa. Naye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alitekeleza amri ya Mola wake Mlezi, na akasimama imara kwenye njia iliyonyooka, mpaka Mwenyezi Mungu akaidhihirisha dini yake kuwa juu ya dini zote, na akamnusuru dhidi ya maadui zake kwa upanga na mkuki baada ya Mwenyezi Mungu kumnusuru kwa hoja na ushindi. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, kama unavyostahiki utukufu wake, ukuu wake, na ukamilifu wake, na upana wa wema wake.
Imetimia Tafsiri ya Surat Yunus, na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.