Yunus
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
قُلْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدْ جَآءَكُمُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنِ ٱهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِى لِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ 108
{108} Yaani, "Sema": Ewe Mtume, wakati ushahidi ulipobainika, "Enyi watu! Haki imekwisha wajia kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, habari ya ukweli inayoungwa mkono na ushahidi, ambayo haina shaka yoyote juu yake kwa namna yoyote ile. Nayo imewafikia kutoka kwa Mola wenu Mlezi ambaye katika malezi yake makubwa zaidi juu yenu ni kwamba aliwateremshia hii Qur'ani ambayo ndani yake kuna ufafanuzi wa kila kitu, na ambayo ndani yake kuna aina mbalimbali za hukumu, na matakwa ya kiungu, na tabia zenye kuridhisha ambayo yote hayo yana malezi makubwa zaidi kwenu. Kwani, uwongofu umeshabainika kutokana na upotofu, na hakuna aliyesalia na shaka yoyote. "Kwa hivyo, anayeongoka" kwa uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kwa kujua haki, na akaifahamu, na akaipendelea juu ya mengineyo, basi ni kwa faida ya nafsi yake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu si mhitaji wa waja wake, bali matunda ya matendo yao yanawarudiwa wao wenyewe. "Na anayepotea" mbali na uwongofu, kwa kupeana mgongo kujua haki au kuifanyia kazi, "basi anapotea kwa hasara ya nafsi yake" wala hamdhuru Mwenyezi Mungu chochote, basi hadhuru isipokuwa nafsi yake mwenyewe. "Na mimi si mwakilishi juu yenu." Basi nikawahifadhia matendo yenu na kuwahesabu juu yake; bali mimi kwenu ni mwonyaji aliye wazi, naye Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi juu yenu. Basi jiangalieni nafsi zenu maadamu bado mko katika kipindi cha kupewa muhula.