Yunus
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
قُلْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمْ فِى شَكٍّ مِّن دِينِى فَلَآ أَعْبُدُ ٱلَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَـٰكِنْ أَعْبُدُ ٱللَّهَ ٱلَّذِى يَتَوَفَّىٰكُمْ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ 104
{104} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - bwana wa Mitume wote, na imamu wa wachamungu, na mbora wa wenye yakini; "Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mko katika shaka juu ya Dini yangu," yaani, katika shaka na kuchanganyikiwa; basi mimi hakika siko katika shaka nayo, lakini nina elimu ya yakini kwamba ndiyo haki, na kwamba hao mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni batili, na nina ushahidi ulio wazi na hoja zinazong'aa juu ya hilo. Na ndiyo maana akasema: "Basi mimi siwaabudu mnaowaabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu" miongoni mwa wenza, na masanamu na wengineo. Kwa sababu hao hawaumbi, wala hawaruzuku, wala hawaendeshi kitu katika mambo, bali hao wameumbwa, wametiishwa, hawana chochote kinachohitaji waabudiwe. "Lakini mimi namwabudu Mwenyezi Mungu anayewafisha." Yaani, yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye aliwaumba, na Yeye ndiye atawafisha, kisha atawafufua ili awalipe kwa matendo yenu. Kwani Yeye ndiye anayestahiki kuabudiwa, na kuswali kwa ajili yake, [na kumnyenyekea] na kusujudiwa. "Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waumini."