İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
Sure 10

Yunus

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

102–103. âyetler

فَهَلْ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثْلَ أَيَّامِ ٱلَّذِينَ خَلَوْا۟ مِن قَبْلِهِمْ ۚ قُلْ فَٱنتَظِرُوٓا۟ إِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُنتَظِرِينَ 102 ثُمَّ نُنَجِّى رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ ٱلْمُؤْمِنِينَ 103

{102 - 103} "Basi, je, wanangojea jingine isipokuwa kama yale yaliyotokea siku za watu waliopita kabla yao?" Yaani, Je, wanangoja hawa wasioamini ishara za Mwenyezi Mungu baada ya kuwa kwake wazi isipokuwa mfano wa siku za wale waliopita kabla yao? Yaani, kuangamizwa na kuadhibiwa. Kwa maana, walifanya kama kufanya kuwao, na desturi ya mwenyezi mungu inapita katika wa mwanzo na mwisho. "Sema: Ngojeni! Nami ni pamoja nanyi katika wanaongoja." Basi Mtakujajua ni nani atakuwa na mwisho mzuri na kuokoka katika dunia na Akhera. Na hayo si isipokuwa kwa Mitume na wafuasi wao tu, na ndio maana akasema: "Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na wale walioamini" kutokana na machukizo ya dunia na Akhera na shida zake. "Ndio kama hivyo, inatustahiki" na tumejiwajibisha juu ya nafsi yetu "kuwaokoa Waumini." Kwa maana, hakika Mwenyezi Mungu huwakinga wale walioamini. Kwani kulingana na imani aliyo nayo mja, ndiyo anapata kuokoka kutokana na machukizo.