Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 92

At-Tawba 9:92

التوبة

وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ إِذَا مَآ أَتَوْكَ لِتَحْمِلَهُمْ قُلْتَ لَآ أَجِدُ مَآ أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ تَوَلَّوا۟ وَّأَعْيُنُهُمْ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمْعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُوا۟ مَا يُنفِقُونَ

Maana

Wala wale wanaokujia ili uwape kipando, ukasema: Sina kipando cha kukubebeeni juu yake, kwa hivyo wanageuka kwenda huku macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kwamba hawatapata cha kutoa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala wale walio kujia ili uwachukue ukasema: Sina kipando cha kukuchukueni. Tena wakarudi na macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa cha kutoa. [92]

[92] Na kadhaalika hapana lawama juu ya Waumini wanao kujia uwapatie kipando cha kwendea Jihadi ukawaambia: Sina cha kukupandisheni. Wakenda zao na macho yao yanatiririka machozi kwa huzuni ya kukosa sharafu ya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa kukosa kwao masurufu ya kutoa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Pia hapana makosa kwa wale ambao wakikujia kutaka uwasaidie kuwachukua kwenda kwenye jihadi, unawaambia, «Sina wanyama wa mimi kuwapatia muwapande», hapo wakakuacha na kugeuka kwenda zao, na macho yao yanabubujika machozi kwa masikitiko ya kukosa utukufu wa jihadi na thawabu zake kwa kuwa hawakupata cha kutumia na cha kuwabeba lau walitoka kwenda kupigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net