At-Tawba 9:91
التوبةلَّيْسَ عَلَى ٱلضُّعَفَآءِ وَلَا عَلَى ٱلْمَرْضَىٰ وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُوا۟ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦ ۚ مَا عَلَى ٱلْمُحْسِنِينَ مِن سَبِيلٍ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Hakuna lawama juu ya wanyonge, wala juu ya wagonjwa, wala juu ya wale wasiopata cha kutoa, maadamu wanamsafia nia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakuna njia ya kuwalaumu wanaofanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapana lawama kwa wanyonge, wagonjwa, na wasio pata cha kutumia, maadamu wanamsafia niya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hapana njia ya kuwalaumu wanao fanya wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [91]
[91] Hakika wanao kubaliwa udhuru wao kubaki nyuma ni wanyonge, na madhaifu wasio jiweza, na wagonjwa, na mafakiri wasio pata cha kutumia kujizatiti kwa vita. Na watu hawa wakiwa wao wana usafi wa niya kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika Dini yao, basi hao ni watu wema, wala hapana lawama juu ya watu wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Maghfira, na Mkunjufu wa Rehema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watu wenye nyudhuru, miongoni mwa madhaifu, wagonjwa na mafukara ambao hawamiliki mali ya kuwawezesha kufanya matayarisho ya kutoka, hawana makosa ya kujikalia, iwapo wamemtakasia Allah Mtukufu na Mtume Wake na wameifuata sheria Yake kivitendo. Hapana njia yoyote kwa wale waliozuiliwa na udhuru kupigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu kupatiwa mateso na kutiwa makosani, iwapo wao ni waaminifu kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake. Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa watenda wema (muhsinûn), ni Mwenye kuwarehemu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net