At-Tawba 9:90
التوبةوَجَآءَ ٱلْمُعَذِّرُونَ مِنَ ٱلْأَعْرَابِ لِيُؤْذَنَ لَهُمْ وَقَعَدَ ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ ۚ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Na walikuja wenye kutoa udhuru miongoni mwa Mabedui ili wapewe ruhusa, na wakakaa wale waliomdanganya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Itawafika wale waliokufuru miongoni mwao adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walikuja wenye kutoa udhuru katika Mabedui ili wapewe ruhusa, na wakakaa wale walio mwambia Mwenyezi Mungu na Mtume wake uwongo. Itawafika walio kufuru katika wao adhabu chungu. [90]
[90] Na kama walivyo bakia nyuma baadhi ya wanaafiki katika Madina wasitoke kwenda pigana Jihadi, kadhaalika walikuja baadhi ya Mabedui, nao ni watu wa majangwani, wakijidai kutoa udhuru huu na huu ili waruhusiwe wabaki nyuma. Na kwa hivyo wakakaa nyuma wale walio mwambia uwongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kuonyesha Imani. Hawakuhudhuria, wala hawakumtaka udhuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ni dalili ya ukafiri wao. Adhabu ya kutia uchungu itawateremkia walio makafiri kati yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kilikuja kikundi, miongoni mwa watu wa vitongoji vya Waarabu wa majangwani, kandokando ya mji wa Madina wakitoa nyudhuru kwa Mtume wa Allah Mtukufu (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), wakimuelezea udhaifu walionao na kutoweza kwao kutoka kwenda vitani. Na kuna watu waliojikalia bila kutoa udhuru wowote kwa kumfanyia ujasiri Mtume wa Allah Mtukufu (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Basi wale waliokufuru miongoni mwa hawa itawatapata adhabu kali, ya kuuawa na nyinginezo hapa duniani, na ya Moto kesho Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net