At-Tawba
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ إِذَا مَآ أَتَوْكَ لِتَحْمِلَهُمْ قُلْتَ لَآ أَجِدُ مَآ أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ تَوَلَّوا۟ وَّأَعْيُنُهُمْ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمْعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُوا۟ مَا يُنفِقُونَ 92
{92} “Wala wale wanaokujia ili uwape kipando” lakini hawakupata kwako kitu “ukasema" ukiwaambia na kupeana udhuru: "Sina kipando cha kuwabebea juu yake, kwa hivyo wanageuka kwenda huku macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kwamba hawatapata cha kutoa.” Kwa maana wao hawana uwezo, wamezitoa nafsi zao, na wamepatwa na huzuni na dhiki kwa yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu kuwahusu. Basi hawa hawana lawama juu yao. Na ikiwa lawama itaondolewa juu yao, basi jambo linarudi katika asili yake; nayo ni kwamba anayekusudia heri na ikaambatana na nia yake thabiti jitihada katika yale anayoweza kufanya, kisha asiweze, basi yeye anachukuliwa kuwa amefanya kikamilifu.