Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 73

At-Tawba 9:73

التوبة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ جَـٰهِدِ ٱلْكُفَّارَ وَٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَٱغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Maana

Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki, na wawiye mgumu. Na makazi yao ni Jahannamu, na hayo ndiyo marejeo mabaya kabisa!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na wakazanie. Na makaazi yao ni Jahannamu, na huo ndio mwisho mbaya. [73]

[73] Ewe Nabii! Shikamana na juhudi ya kuwazuia makafiri na ukafiri wao, na wanaafiki na unaafiki wao. Na wakazanie katika juhudi yako. Makaazi yao hawa aliyo waahidi Mwenyezi Mungu huko Akhera ni Jahannamu. Na uovu ulioje mwisho huo!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii! Pigana vita na makafiri kwa upanga, na wanafiki kwa ulimi na kusimamisha hoja, na ukazane juu ya hayo mapote mawili. Na mahala pao pa kutulia ni Motoni; na ubaya wa mahala pa kuishia ni hapo watakapoishia wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net