At-Tawba 9:72
التوبةوَعَدَ ٱللَّهُ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا وَمَسَـٰكِنَ طَيِّبَةً فِى جَنَّـٰتِ عَدْنٍ ۚ وَرِضْوَٰنٌ مِّنَ ٱللَّهِ أَكْبَرُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ
Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Bustani zipitiazo mito chini yake, watadumu humo. Na makazi mema katika Bustani za kudumu, na Radhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ndizo kubwa zaidi kuliko yote. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na makaazi mema katika Bustani za kudumu, na Radhi za Mwenyezi Mungu ndio kubwa kuliko yote. Huko ndiko kufuzu kukubwa. [72]
[72] Mwenyezi Mungu amewaahidi hao Bustani (Pepo) watakao kaa daima katika neema zake, na makaazi ya kuziliwaza nafsi zao katika makao ya kudumu milele. Na pamoja na hayo watapata Radhi ya Mwenyezi Mungu kuwa radhi nao, nayo wataiona. Na hiyo ndiyo neema kubwa kabisa. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amewaahidi wenye kumuaumini Allah Mtukufu na Mtume Wake, waume na wake, mabustani ya Pepo ambayo chini yake inapita mito, hali ya kukaa humo milele. Starehe zake Haziwaondokei, yana majumba yaliyojengwa vizuri yenye utulivu mzuri katika mabustani ya makao. Na radhi itokayo kwa Allah Mtukufu watakayoipata ni kubwa zaidi na ni bora zaidi kuliko starehe walizonazo. Ahadi hiyo ya malipo mema ya Akhera ndio kufaulu kukubwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net