Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 71

At-Tawba 9:71

التوبة

وَٱلْمُؤْمِنُونَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَيُطِيعُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ ٱللَّهُ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Maana

Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na husimamisha Sala, na hutoa Zaka, na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [71]

[71] Na Waumini wanaume na Waumini wanawake, wao kwa wao ni wapenzi wa kupendana na kusaidiana, kwa mujibu wa Imani. Wanaamrisha yanayo amrishwa na Dini yao ya Haki, na wanakataza yanayo katazwa na Dini. Wanatimiza Swala kwa nyakati zake, wanatoa Zaka kuwapa wanao stahiki kwa wakati wake. Na wanat'ii anayo waamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na wanayaepuka anayo yakataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hao ndio watakao kuwa chini ya Rehema ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwalinda kwa Rehema, na Mwenye hikima katika upaji wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, waume na wake, wanasaidiana wao kwa wao, wanaamrisha watu kuamini na kufanya vitendo vyema na wanawakataza kukanusha na kufanya maasia, wanatekeleza Swala, wanatoa Zaka, wanamtii Allah Mtukufu na Mtume Wake na wanakomeka kufanya yale waliyokatazwa. Hao Allah Mtukufu Atawarehemu, Atawaokoa na adhabu Yake na Atawatia Peponi. Hakika Allah Mtukufu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake na hukumu Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net