At-Tawba 9:70
التوبةأَلَمْ يَأْتِهِمْ نَبَأُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَقَوْمِ إِبْرَٰهِيمَ وَأَصْحَـٰبِ مَدْيَنَ وَٱلْمُؤْتَفِكَـٰتِ ۚ أَتَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ ۖ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ
Je, hazikuwajia habari za wale waliokuwa kabla yao, kaumu ya Nuhu, na A'ad, na Thamud, na kaumu ya Ibrahim, na watu wa Madyana, na miji iliyopinduliwa chini juu? Mitume wao waliwajia na hoja zilizo wazi. Basi Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, hazikuwafikia khabari za walio kuwa kabla yao - kaumu ya Nuhu, na A'ad, na Thamud, na kaumu ya Ibrahim, na watu wa Madyana, na miji iliyo pinduliwa chini juu? Mitume wao waliwafikia kwa hoja zilizo wazi. Basi Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, walakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe. [70]
[70] Basi je, hawazingatii wanaafiki na makafiri hali ya walio watangulia katika kaumu ya Nuhu na A'ad na Thamud na kaumu ya Ibrahim na kaumu ya Shuaib na kaumu Lut'? Mitume wa Mwenyezi Mungu waliwajia na hoja zilizo wazi wazi kutokana na Mwenyezi Mungu, na wakawakanusha na wakawakataa! Mwenyezi Mungu akawashika kila mmoja wao kwa dhambi zake, na akawateketeza wote! Wala Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walizidhulumu wenyewe nafsi zao kwa ukafiri wao, na uasi wao kumuasi Mwenyezi Mungu, na wakastahiki peke yao kupata adhabu. Basi wao ndio wanao jidhulumu wenyewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani haikuwajia wanafiki hawa habari ya wale waliopita, miongoni mwa watu wa Nûḥ, kabila la ‛Ãd, kabila la Thamûd, watu wa Ibrãhîm, watu wa Madyan na watu wa Lûṭ, walipowajia Mitume na wahyi na aya za Allah Mtukufu wakawakanusha? Wote hawa Allah Mtukufu Aliwateremshia adhabu Yake, kuwalipiza wao kwa matendo yao mabaya. Allah Mtukufu Hakuwa ni mwenye kuwadhulumu, lakini ni wao wenyewe walijidhulumu nafsi zao kwa kukanusha na kupinga.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net