Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 69

At-Tawba 9:69

التوبة

كَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوٓا۟ أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَٰلًا وَأَوْلَـٰدًا فَٱسْتَمْتَعُوا۟ بِخَلَـٰقِهِمْ فَٱسْتَمْتَعْتُم بِخَلَـٰقِكُمْ كَمَا ٱسْتَمْتَعَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَـٰقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَٱلَّذِى خَاضُوٓا۟ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ

Maana

Ni kama wale waliokuwa kabla yenu. Walikuwa wana nguvu na mali na watoto zaidi kuwaliko nyinyi. Basi walistareheka kwa fungu lao, na nyinyi mnastareheka kwa fungu lenu, kama walivyostareheka kwa fungu lao wale waliokuwa kabla yenu. Na nyinyi mkazama katika maovu kama wao walivyozama. Hao, matendo yao yaliharibika katika dunia na Akhera; na hao ndio waliohasiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ni kama wale walio kuwa kabla yenu. Walikuwa wana nguvu na mali na watoto zaidi kuliko nyinyi. Basi walistarehea fungu lao, na nyinyi mnastarehea fungu lenu, kama walivyo starehe kwa fungu lao wale walio kuwa kabla yenu. Na nyinyi mkazama katika maovu kama wao walivyo zama. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika katika dunia na Akhera; na hao ndio walio khasiri. [69]

[69] Hakika hali yenu, enyi wanaafiki, ni kama hali ya wenzenu walio kutangulieni katika unaafiki na ukafiri. Kwa hakika wao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko nyinyi, na walikuwa na mali zaidi na watoto. Wakajistarehea kwa sehemu yao ya dunia walio jaaliwa, na wakapuuza kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kumcha Yeye. Na wakawakabili Manabii wao kwa kuwabeua na kuwakejeli. Na nyinyi mmejistarehea vile vile kwa mlivyo jaaliwa katika ladha za kidunia, kama walivyo jistarehea wao. Na nyinyi mkabobea katika mambo machafu na mapotovu kama walivyo bobea wao. Hakika hao vitendo vyao vimeharibika, basi havikuwafaa duniani wala Akhera, na wakawa wenye kukhasiri. Na nyinyi ni mfano wa hao katika hali na matokeo maovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika vitendo vyenu, enyi wanafiki, vya kucheza shere na ukafiri ni kama vitendo vya watu waliotangulia, waliokuwa na nguvu nyingi na mali na watoto zaidi kushinda nyinyi, wakajiimarisha na maisha ya kilimwengu, wakasterehe na vitu na ladha zilizomo. Basi na nyinyi, enyi wanafiki, mumestarehe kwa sehemu yenu ya matamanio yenye kumalizika kama starehe ya waliokuwa kabla yenu kwa mafungu yao ya vitu vya kilimwengu vyenye kumalizika. Na mumejiingiza katika kumzulia Allah Mtukufu urongo kama walivyojiingiza wale watu waliokuwa kabla yenu. Hao wenye kusifiwa kwa tabia hizi, ndio wale ambao mema yao yameondoka duniani na Akhera. Na wao ndio wenye kupata hasara kwa kuuza kwao starehe za Akhera kwa vyeo na starehe za ulimwenguni.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net