At-Tawba 9:68
التوبةوَعَدَ ٱللَّهُ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَٱلْمُنَـٰفِقَـٰتِ وَٱلْكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ هِىَ حَسْبُهُمْ ۚ وَلَعَنَهُمُ ٱللَّهُ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ
Mwenyezi Mungu amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahannamu watadumu humo. Hiyo ndiyo inawatosha, na Mwenyezi Mungu amewalaani; nao wana adhabu ya kudumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu amewaahidi wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahannamu kudumu humo. Hayo yanawatosha, na Mwenyezi Mungu amewalaani; nao wana adhabu milele. [68]
[68] Mwenyezi Mungu amewaandikia wanaafiki na makafiri Moto wa Jahannamu. Atawaadhibu humo, wala hawatatoka. Hayo yanatosha kuwa ni malipo yao, na pamoja na malipo hayo watapata kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu na adhabu ya daima Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amewaahidi wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike na Makafiri kwamba mwisho wao ni kwenda kwenye Moto wa Jahanamu, wakae humo milele kabisa. Moto huo ni wenye kuwatosha, ukiwa ni mateso yao kwa kumkanusha kwao Allah Mtukufu. Na Allah Mtukufu Amewafukuza kwenye rehema zake. Na watakua na adhabu ya daima.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net