At-Tawba 9:67
التوبةٱلْمُنَـٰفِقُونَ وَٱلْمُنَـٰفِقَـٰتُ بَعْضُهُم مِّنۢ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِٱلْمُنكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمَعْرُوفِ وَيَقْبِضُونَ أَيْدِيَهُمْ ۚ نَسُوا۟ ٱللَّهَ فَنَسِيَهُمْ ۗ إِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ
Wanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wote ni hali moja. Huamrisha maovu na hukataza mema, na huifumba mikono yao. Walimsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia akawasahau. Hakika wanafiki ndio wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanaume wanaafiki na wanawake wanaafiki, wote ni hali moja. Huamrisha maovu na huyakataza mema, na huifumba mikono yao. Wamemsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia amewasahau. Hakika wanaafiki ndio wapotofu. [67]
[67] Wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake wamefanana kwa kuwa wote wanatenda maovu, na wanayaamrisha, na wanaiacha Haki na wanaikataza, na wanafanya ubakhili kutumia mali katika njia za kheri. Basi hao kama ni viungo vya mwili mmoja. Wamemwacha Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu naye akawaacha wala hawaongoi, kwa kuwa wao wamekwisha toka kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike ni aina moja katika kutangaza kwao Imani na kuficha kwao ukafiri. Wanaamrisha kukufuriwa Allah Mtukufu na kuasiwa Mtume Wake, na wanakataza Imani na utiifu, na wanaizuia mikono yao kutoa katika njia ya Allah Mtukufu. Wamemsahau Allah Mtukufu na kwa hivyo hawamtaji, na Yeye Amewasahau na rehema Yake hakuwaelekeza kwenye wema. Hakika wanafiki ndio waliotoka nje wakaacha kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net