Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 66

At-Tawba 9:66

التوبة

لَا تَعْتَذِرُوا۟ قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَـٰنِكُمْ ۚ إِن نَّعْفُ عَن طَآئِفَةٍ مِّنكُمْ نُعَذِّبْ طَآئِفَةًۢ بِأَنَّهُمْ كَانُوا۟ مُجْرِمِينَ

Maana

Msitoe udhuru. Hakika mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja miongoni mwenu, tunaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao wamekuwa wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu. [66]

[66] Msitoe udhuru kama huu wa uwongo! Ukafiri wenu umekwisha dhihiri baada ya kujidai kwenu kuwa mmeamini. Na ikiwa Sisi tutalisamehe kundi moja lenu lilio tubu na likaamini, kwa sababu ya kutubu kwake kwa kweli, na kuamini kwake, vile vile tutaliadhibu kundi jengine katika nyinyi kwa kushikilia kwake ukafiri na unaafiki, na ukhalifu wake katika haki ya Mtume na ya Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Msitoe sababu, enyi mkusanyiko wa wanafiki! Kwani hakuna faida ya kutoa udhuru kwenu. Hakika mmekufuru kwa maneno haya mliyoyafanyia shere. Iwapo tutalisamehe kundi miongoni mwenu lililotaka msamaha na likatubia kidhati, tutaliadhibu kundi la watu wengine kwa sababu ya uhalifu wao wa kusema maneno haya maovu ya makosa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net