Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 64

At-Tawba 9:64

التوبة

يَحْذَرُ ٱلْمُنَـٰفِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيْهِمْ سُورَةٌ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِى قُلُوبِهِمْ ۚ قُلِ ٱسْتَهْزِءُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ مُخْرِجٌ مَّا تَحْذَرُونَ

Maana

Wanafiki wanaogopa kwamba iteremshwe Sura juu yao itakayowaambia yale yaliyo katika nyoyo zao. Sema: Fanyeni stihizai! Hakika Mwenyezi Mungu atayatoa nje hayo mnayoyaogopa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanaafiki wanaogopa isije teremshwa Sura itakayo watajia yaliyomo katika nyoyo zao. Sema: Fanyeni mzaha! Hakika Mwenyezi Mungu atayatoa nje hayo mnayo yaogopa. [64]

[64] Wanaafiki wanapo kuwa wao kwa wao humfanyia kejeli Mtume, na wao wanaogopa yasifedheheke mambo yao, zikamteremkia Nabii Aya za Qur'ani zitakazo fichua yale wanayo yaficha katika nyoyo zao, na wanayafanya ni siri baina yao! Ewe Mtume! Waambie: Fanyeni maskhara yenu mpendavyo, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyafichua hayo mnayo yaogopea yasije kudhihiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wanafiki wanaogopa kuteremshwa sura kuhusu wao, yenye kuwapa habari ya ukafiri waliouficha ndani ya nyoyo zao. Waambie, ewe Nabii, Endeleeni juu ya yale ambayo mko nayo ya kufanya shere na masihara. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kuutoa nje ukweli wa yale mliokuwa na hadhari nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net