Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 63

At-Tawba 9:63

التوبة

أَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّهُۥ مَن يُحَادِدِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَأَنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدًا فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ ٱلْخِزْىُ ٱلْعَظِيمُ

Maana

Je, hawajui ya kwamba anayempinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo hakika ana Moto wa Jahannam adumu humo? Hiyo ndiyo hizaya kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, hawajui ya kwamba anaye shindana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo atapata Moto wa Jahannamu adumu humo? Hiyo ndiyo hizaya kubwa. [63]

[63] Hivyo hawa wanaafiki hawajui kwamba malipo ya mwenye kumkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akashindana nao ni adhabu ya daima katika Moto wa Jahannamu? Na hiyo ndiyo hizaya ya kufedhehesha, na madhila makubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawakujua wanafiki hawa kwamba mwisho wa wale wanaompiga vita Allah Mtukufu na Mtume Wake ni Moto wa Jahanamu, watakuwa na adhabu kali ndani yake? Mwisho huo ndio utwevu na unyonge mkubwa. Na miongoni mwa kupiga vita kwao huko ni kumkera Mtume wa Allah Mtukufu (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa kumtukana na kumtia dowa; Allah Mtukufu Atulinde na hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net