At-Tawba 9:62
التوبةيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمْ لِيُرْضُوكُمْ وَٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَحَقُّ أَن يُرْضُوهُ إِن كَانُوا۟ مُؤْمِنِينَ
Wanawaapia kwa Mwenyezi Mungu ili wakuridhishenyi, ilhali Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaostahiki zaidi kwamba wao wawaridhishe ikiwa wao ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanakuapieni Mwenyezi Mungu ili kukuridhisheni nyinyi, hali ya kuwa wanao stahiki zaidi kuridhishwa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake, lau kama wao ni Waumini. [62]
[62] Katika kwenda vitani wao hubaki nyuma hawatoki nanyi kwenda kupigana na adui zenu wala hawataradadi. Na kisha hukutoleeni udhuru wa uwongo kwa kule kubaki kwao nyuma. Na hukuapieni ili muwaridhie na mkubali udhuru wao. Na wa kustahiki kutakiwa radhi kama wao kweli ni Waumini, ni Mwenyezi Mungu na Mtume.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanafiki wanaapa viapo vya urongo na wanatoa nyudhuru za kupanga ili kuwafanya Waumini waridhike na wao. Na Allah Mtukufu na Mtume Wake wanastahiki zaidi na inafaa zaidi wawaridhie kwa kuwaamini na kuwatii, iwapo kweli wao ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net