At-Tawba 9:61
التوبةوَمِنْهُمُ ٱلَّذِينَ يُؤْذُونَ ٱلنَّبِىَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ ۚ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ ۚ وَٱلَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ ٱللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Na miongoni mwao kuna wale wanaomuudhi Nabii na wanasema: Yeye ni sikio tu. Sema: Basi ni sikio la heri kwenu. Anamwamini Mwenyezi Mungu, na ana imani na Waumini, naye ni rehema kwa wanaoamini miongoni mwenu. Na wale wanaomuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu wana adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na miongoni mwao wapo wanao muudhi Nabii na kusema: Yeye huyu ni sikio tu. Sema: Basi ni sikio la kheri kwenu. Anamuamini Mwenyezi Mungu, na ana imani na Waumini, naye ni rehema kwa wanao amini miongoni mwenu. Na wanao muudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watapata adhabu chungu. [61]
[61] Na wapo watu wanaafiki wanakusudia kumuudhi Nabii, na kumletea ya kumkirihi. Wao humtuhumu kuwa anapenda kusikiliza kila analo ambiwa, kweli na uwongo, na kwamba yeye anakhadaika na hayo anayo yasikia. Basi, ewe Mtume! Waambie: Huyo mnaye msengenya nyuma yake sio kama mnavyo dai. Bali yeye ni sikio la kheri kwenu. Hasikii ila la kweli, wala hakhadaiki na upotovu. Anamsadiki Mwenyezi Mungu na wahyi (ufunuo) wake, na anawasadiki Waumini, kwa sababu Imani yao inawakataza uwongo. Na yeye ni rehema kwa kila mmoja wenu anaye amini. Na hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia wanao muudhi Mtume adhabu chungu, na kali, na ya kudumu milele.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa wanafiki kuna watu wanaomkera Mtume wa Allah Mtukufu kwa maneno na wanasema, «Yeye anasikiliza kila aambiwalo na analiamini.» Waambie, Muhammad ni sikio linalosikiliza kila jema. Anamuamini Allah Mtukufu na anawasadiki Waumini kwa yale wanayomwambia. Na yeye ni rehema kwa aliyemfuata na akaongoka kwa uongofu Wake. Na wenye kumkera Mtume wa Allah Mtukufu, Muhammad (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa namna yoyote ya kumkera, watakuwa na adhabu yenye kuumiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net