Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 39

At-Tawba 9:39

التوبة

إِلَّا تَنفِرُوا۟ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْـًٔا ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Kama hamuendi, atawaadhibu adhabu chungu, na atawabadilisha na kaumu wasiokuwa nyinyi, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. [39]

[39] Msipo muitikia Mtume, mkatoka nje kwenda pigana Jihadi, Mwenyezi Mungu atakupeni adhabu iliyo chungu, na Mola wenu Mlezi atawabadilisha watu waje wengine, sio nyinyi, wamuitikie Mtume wala hawatobaki nyuma ikinadiwa Jihadi. Wala nyinyi kwa kukataa kwenu kwenda pigana, hamtamdhuru Mwenyezi Mungu chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo mkubwa juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Iwapo hamtatoka, enyi Waumini, kwenda kupigana na adui yenu, Allah Mtukufu Atawateremshia mateso Yake na atawaleta watu wengine ambao watatoka kwenda vitani waambiwapo watoke, watamtii Allah Mtukufu na Mtume Wake. Na nyinyi hamtamdhuru Allah Mtukufu chochote kwa kuikimbia kwenu jihadi, kwani Yeye ni mwenye kujitosheleza na nyinyi, na nyinyi ndio wahitaji Wake. Na Analolitaka Allah Mtukufu litakuwa hapana budi. Na Allah Mtukufu, juu ya kila kitu, ni Muweza, miongoni mwa kutetea dini Yake na Mtume Wake pasi na nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net