Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 38

At-Tawba 9:38

التوبة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ٱنفِرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱثَّاقَلْتُمْ إِلَى ٱلْأَرْضِ ۚ أَرَضِيتُم بِٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا مِنَ ٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ فَمَا مَتَـٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ

Maana

Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kwa kulinganisha na Akhera siyo isipokuwa chache.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. [38]

[38] Enyi Waumini! Mna nini, anapo kwambieni Mtume: Tokeni mwende kwenye Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baadhi yenu mkafanya uzito kutoka? Haikufalieni hivyo! Mnaona afadhali maisha ya dunia yatayo kwisha, kuliko maisha ya Akhera na neema zake za kudumu? Starehe ya duniani na utamu wake ukilinganisha na starehe ya Akhera ni chache na upuuzi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na Mkafuata sheria Zake kivitendo, mna nini nyinyi pindi mkiambiwa, «Tokeni muende jihadi katika njia ya Allah Mtukufu ili mkapigane na maadui wenu,» mnafanya uvivu na mnajikalia majumbani mwenu? Je mnapendelea mafungu yenu ya starehe za kilimwengu kuliko neema za kesho Akhera? Basi kile mnachostarehe nacho ulimwenguni ni kichache chenye kuondoka. Ama neema za Akhera ambazo Allah Mtukufu Ameziandalia Waumini ni nyingi zenye kudumu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net