At-Tawba 9:36
التوبةإِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّهُورِ عِندَ ٱللَّهِ ٱثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِى كِتَـٰبِ ٱللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ مِنْهَآ أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا۟ فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَـٰتِلُوا۟ ٱلْمُشْرِكِينَ كَآفَّةً كَمَا يُقَـٰتِلُونَكُمْ كَآفَّةً ۚ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُتَّقِينَ
Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na miwili katika andiko la Mwenyezi Mungu tangu alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko minne mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wanavyopigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu. [36]
[36] Hakika hisabu ya miezi ya kuandama ni miezi kumi na mbili, kwa hukumu na kudra ya Mwenyezi Mungu, na ndivyo alivyo ibainisha katika vitabu vyake tangu kuanza ulimwengu. Na katika hii miezi thinaashara (kumi na mbili) ipo mine imekatazwa kupigana vita ndani yake, nayo:-Mwezi wa Rajab, Alqa'ada (Mfungo Pili), Alhijja (Mfungo Tatu), na Almuharram (Mfungo Nne). Na huku kuitukuza miezi hii mine na kuharimisha kupigana vita ndani yake ndiyo Dini ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka, ambayo haibadiliki wala haina mageuzo. Basi msijidhulumu nafsi zenu kwa kuhalalisha vita katika miezi hii, au mkaacha kujilinda adui akikupigeni. Na enyi Waumini! Piganeni na washirikina bila ya kumbagua yeyote kati yao, kama wanavyo kupigeni nyinyi nyote. Na kuweni na yakini kuwa Mwenyezi Mungu atawanusuru wanao mcha, na wakashika amri zake, na wakaepuka anayo yakataza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika idadi ya miezi, katika hukumu ya Allah Mtukufu na kulingana na ilivyoandikwa kwenye al-Lawḥ al-Maḥfûẓ (Ubao uliohifadhiwa), ni miezi kumi na mbili, tangu siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo, kuna minne mitakatifu ambayo Allah Mtukufu Ameharamisha ndani yake kupigana. Nayo ni Mfungopili, Mfungotatu, Mfungo nne na Rajabu. Hiyo ndio Dini ilionyooka sawa. Basi ndani ya miezi hiyo msizidhulumu nafsi zenu, kwa kuwa uharamu wake umeongezwa. Na kwa kuwa kudhulumu katika miezi hiyo ni kubaya zaidi kuliko katika miezi mingineyo, haina maana kwamba kudhulumu katika miezi mingine kunaruhusiwa. Na wapigeni vita washirikina wote kama wanavyowapiga vita nyote. Na mjue kwamba Allah Mtukufu Yuko pamoja na wenye taqwã (uchajimungu) kwa msaada Wake na nusura Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net