Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 35

At-Tawba 9:35

التوبة

يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِى نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا۟ مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ

Maana

Siku zitakapotiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mliyozilimbikia nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkilimbika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku zitapo tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu, basi onjeni mliyo kuwa mkilimbika. [35]

[35] -- Siku ya Kiyama, kwa kuwa hayo mali yatatiwa kwenye Moto wa Jahannamu, kisha waunguzwe nayo kwenye vipaji vya nyuso zao, na mbavu zao, na migongo yao; na waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkijilimbikia kama khazina kwa ajili ya nafsi zenu, wala hamkuwa mkitoa haki ya Mwenyezi Mungu! Basi ionjeni hii leo adhubu kali!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Siku ya Kiyama yatawekwa mapande ya dhahabu na fedha kwenye Moto, na yatakaposhika moto sana, watachomwa nayo, hao wenyewe, nyuso zao, mbavu zao na migongo yao. Na wataambiwa kwa kuwaumbua, Haya ndiyo mali yenu mliyoyakumbatia na mkazuia, katika mali hayo, haki za Allah Mtukufu. Basi onjeni adhabu iumizayo, kwa sababu ya kukusanya kwenu na kuzuia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net