At-Tawba 9:34
التوبةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْأَحْبَارِ وَٱلرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلْبَـٰطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۗ وَٱلَّذِينَ يَكْنِزُونَ ٱلذَّهَبَ وَٱلْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Enyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wale wanaolimbika dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, basi wabashirie adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa baat'ili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu. [34]
[34] Enyi Waumini! Jueni kuwa wengi katika wataalamu wa Kiyahudi na mapadri wa Kikristo wanajihalalishia kula mali ya watu bila ya haki yoyote, na wanawazuga wafwasi wao wanao waamini kwa kila walisemalo. Na wanawazuilia watu wasiingie katika Uislamu. Na wale wanao kusanya mali, dhahabu na fedha, wakiyaweka tu, wala hawatoi Zaka zake, waonye ewe Mtume, kuwa kuna adhabu ya kutia uchungu _
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, hakika wengi wa wanavyuoni wa watu waliopewa Vitabu na watu wema wao wanakula mali za watu kwa njia isiyokuwa ya haki, kama hongo na vinginevyo, na wanakataza watu wasiingie kwenye Uislamu na wanazuia njia ya Allah Mtukufu isifuatwe. Na wale wanaozuia mali wakawa hawatekelezi Zaka zake wala hawatoi katika mali hizo haki za lazima, basi wape bishara ya adhabu iumizayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net