Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 33

At-Tawba 9:33

التوبة

هُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلْهُدَىٰ وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْمُشْرِكُونَ

Maana

Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili aipe ushindi juu ya dini zote, hata washirikina wakichukia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia. [33]

[33] Yeye ndiye Mwenyezi Mungu aliye dhamini kutimiza Nuru yake kwa kumtuma Mtume wake, Muhammad s.a.w. na hoja zilizo wazi, na Dini ya Haki, Uislamu, ipate kutukuka Dini hii juu ya dini zote zilizo tangulia, ijapo kuwa washirikina watakasirika. Mwenyezi Mungu ataipa ushindi tu, wakitaka wasitake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yeye Ndiye Aliyemtuma Mtume Wake Muhammad (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa Qur’ani na dini ya Uislamu, ili Aifanye kuwa juu ya dini zote, ingawa washirikina wanaichukia dini ya haki- Uislamu- na kushinda kwake dini nyingine.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net