Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 32

At-Tawba 9:32

التوبة

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِـُٔوا۟ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفْوَٰهِهِمْ وَيَأْبَى ٱللَّهُ إِلَّآ أَن يُتِمَّ نُورَهُۥ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْكَـٰفِرُونَ

Maana

Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa aitimize Nuru yake hata makafiri wakichukia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. [32]

[32] Makafiri wanataka kwa madai yao ya upotovu waizime Nuru ya Mwenyezi Mungu, nayo ni Uislamu. Na Mwenyezi Mungu hataki ila aitimize Nuru yake, kwa kuidhihirisha Dini yake na ashinde Mtume wake, ijapo kuwa wao watachukia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Makafiri, kwa kukanusha kwao, wanataka kuuzima Uislamu na kuzizima hoja za Allah Mtukufu na dalili Zake, juu ya upweke Wake, Alizokuja nazo Muhammad (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Na Allah Mtukufu Anakataa isipokuwa kuikamilisha dini Yake na kuipa nguvu, na kuliinua neno Lake, hata kama wenye kukanusha watalichukia hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net