Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 31

At-Tawba 9:31

التوبة

ٱتَّخَذُوٓا۟ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَـٰنَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَٱلْمَسِيحَ ٱبْنَ مَرْيَمَ وَمَآ أُمِرُوٓا۟ إِلَّا لِيَعْبُدُوٓا۟ إِلَـٰهًا وَٰحِدًا ۖ لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Maana

Waliwafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni mabwana badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi mwana wa Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Mungu Mmoja, hakuna mungu isipokuwa Yeye. Subhanahu (ametakasika) mbali na hayo wanayoyashirikisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo. [31]

[31] Hao Mayahudi na Wakristo wamewafanya makuhani wao na mapadri kuwa ni "Marabi", kama ni miungu, kwa kuwapa madaraka ya kutunga sharia, na kuwa maneno yao ndiyo dini, ijapo kuwa yanakhitalifiana na kauli za Mtume wao. Wanawafuata katika upotovu wao, na wakamuabudu Masihi mwana wa Maryamu! Na Mwenyezi Mungu amewaamrisha katika hivyo hivyo Vitabu vyao kwa ndimi za Mitume wao, kuwa wasimuabudu ila Mungu Mmoja, kwa kuwa Yeye hapana anaye stahiki kuabudiwa kwa mujibu wa hukumu ya sharia na akili ila Mungu Mmoja. Mwenyezi Mungu ametakasika na kushirikishwa katika ibada, uumbaji, na sifa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mayahudi na Wanaswara wamewafanya wanavyuoni na watu wema kuwa ni waungu wenye kuwawekea hukumu za sheria, wakawa wanajilazimisha kuzifuata na wanaacha sheria za Allah Mtukufu. Na pia walimfanya Al-Masîḥ, ‘Ǐsâ mwana wa Maryam, kuwa ni mungu, wakamuabudu. Na hakika Allah Mtukufu Amewaamrisha wao wamuabudu Yeye Peke Yake, bila ya mwingine. Yeye Ndiye Mungu wa haki. Hakuna mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Amejiepusha na Ametakasika na kila kile wanachokizua watu wa ushirikina na upotevu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net