At-Tawba 9:30
التوبةوَقَالَتِ ٱلْيَهُودُ عُزَيْرٌ ٱبْنُ ٱللَّهِ وَقَالَتِ ٱلنَّصَـٰرَى ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ ٱللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَٰهِهِمْ ۖ يُضَـٰهِـُٔونَ قَوْلَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَبْلُ ۚ قَـٰتَلَهُمُ ٱللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
Na Mayahudi walisema: Uzeir ni mwana wa Mwenyezi Mungu. Na Wakristo walisema: Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ni kauli yao tu kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa! [30]
[30] Mayahudi wameacha Tawhidi, ya kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja pekee, na wakasema kuwa Uzair ni mwana wa Mungu! (Mayahudi wa Arabuni tu ndio walimfanya Uzair ni mwana wa Mungu.) Na Wakristo nao wakaacha Imani ya Mungu Mmoja vile vile, wakasema: Masihi ni mwana wa Mungu!! Na kauli yao hii ni ya uzushi, wanakariri kwa vinywa vyao, wala hayakuletwa hayo na Kitabu wala Mtume. Wala hawana hoja wala ushahidi wa hayo. Na katika haya wanafanana na maneno ya washirikina walio kuwa kabla yao! Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri hawa, na atawaangamiza! Ama ajabu watu hawa! Vipi wanaipotea Haki nayo ni dhaahiri inaonekana, na wanakwenda kufuata upotovu!! Uzair ndiye Ezra, Kuhani katika ukoo wa Harun. Alitoka Babilonia walipo rejea Mayahudi mara ya pili, baada ya kufa Mtume wa Mwenyezi Mungu Musa, a.s. kwa kiasi ya miaka elfu. Na huyo Uzair akiitwa "Katibu" kwa kuwa alikuwa akiandika Sharia ya Musa. Angalia: Uzair pamoja na Mayahudi wengine walitoka huko Babilonia kwendea Yerusalemu katika mwaka 456 K.K. (Kabla ya Kristo) katika enzi ya Arikhtisna, Mfalme wa Iran baada ya kuteketezwa Yerusalemu na kuunguzwa Baitul Muqaddas na kunajisiwa kwa muda mrefu
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wamemshirikisha Allah Mtukufu Mayahudi walipodai kwamba ‛Uzayr ni mwana wa Allah Mtukufu. Na wamemshirikisha Allah Mtukufu Wanaswara walipodai kwamba Al-Masîh ni mwana wa Allah Mtukufu, Neno hili wamelizua wao wenyewe, na wao kwa hili wanafananisha na neno la washirikina kabla yao. Allah Mtukufu Awalaani washirikina wote. Vipi wao wajiepusha na ukweli na kuelekea kwenye urongo?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net