Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 28

At-Tawba 9:28

التوبة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّمَا ٱلْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا۟ ٱلْمَسْجِدَ ٱلْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦٓ إِن شَآءَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu. Na ikiwa mnahofia umasikini, basi Mwenyezi Mungu atakutajirisheni kutoka katika fadhila zake akitaka. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Hakika washirikina ni najsi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu. Na ikiwa mnakhofia umasikini, basi Mwenyezi Mungu atakutajirisheni kwa fadhila yake akipenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. [28]

[28] Enyi Waumini! Washirikina kwa sababu ya ushirikina wao wamejinajisi nafsi zao, nao wamepotea katika itikadi. Msiwaachilie kuingia Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka huu (9 Hijra). Mkichelea ufakiri kwa kukatika biashara Mwenyezi Mungu atakupeni badala yake, na atakutoshelezeni kwa fadhila yake akipenda. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua mambo yenu yote, na Mwenye hikima katika mipango yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mkusanyiko wa Waumini, hakika washirikina ni najisi na ni wachafu, hivyo basi msiwape nafasi kusongea kwenye eneo la Ḥaram baada ya mwaka huu wa tisa wa hijria (kalenda ya Kiislamu). Na iwapo mtachelea umasikini, kwa kukatikiwa na biashara zao, Allah Mtukufu Atawapa badala yake na Atawatosheleza kwa fadhila Zake Atakapo. Hakika Allah Mtukufu ni Mjuzi mno wa hali zenu, ni Mwingi wa hekima katika kuyapeleka mambo yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net