Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 27

At-Tawba 9:27

التوبة

ثُمَّ يَتُوبُ ٱللَّهُ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu atamkubalia toba amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu atawasamehe awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [27]

[27] Kisha Mwenyezi Mungu atakubali toba ya amtakaye katika waja wake, na amsamehe dhambi zake, pindi akirejea kwa usafi wa moyo. Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kusamehe, Mkuvunjufu wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na atakayerudi nyuma akaacha ukafiri wake baada ya hilo, na akaingia kwenye Uislamu, basi Allah Mtukufu Anaikubali toba ya Anayemtaka katika wao na Anamsamehe dhambi zake. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe, ni mwingi wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net