Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 26

At-Tawba 9:26

التوبة

ثُمَّ أَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا وَعَذَّبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya Waumini. Na akateremsha majeshi ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru. Na hayo ndiyo malipo ya makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya Waumini. Na akateremsha majeshi ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale walio kufuru. Na hayo ndiyo malipo ya makafiri. [26]

[26] Tena mkapata himaya ya Mwenyezi Mungu. Akateremsha utulivu juu ya Mtume wake, na akaujaza utulivu katika nyoyo za Waumini, na akakuungeni mkono kwa Malaika, jeshi lake, walio tia imara miguu yenu. Nanyi hamkuwaona Malaika hao...Na Mwenyezi Mungu akawaonjesha maadui zenu machungu ya kushindwa. Na hayo ndiyo malipo ya makafiri duniani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha Allah Mtukufu Alimteremshia utulivu Mtume Wake na Waumini wakasimama imara, na Allah Mtukufu Akawaongezea askari wasiowaona miongoni mwa Malaika. Hapo Aliwapa ushindi juu ya adui yao na akawaadhibu wale waliokufuru. Hayo ni mateso ya Allah Mtukufu kwa wenye kuzuia dini ya Allah Mtukufu isifuatwe, wenye kuwakanusha Mitume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net