Al-Anfaal 8:6
الأنفاليُجَـٰدِلُونَكَ فِى ٱلْحَقِّ بَعْدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى ٱلْمَوْتِ وَهُمْ يَنظُرُونَ
Wanakujadili kuhusu haki baada ya kwisha bainika, kama kwamba wanasukumwa kwenye mauti hali ya kuwa wanatazama.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanajadiliana nawe kwa jambo la Haki baada ya kwisha bainika, kama kwamba wanasukumwa kwenye mauti nao wanaona. [6]
[6] Wanajadiliana nawe hao wa kikundi hicho, na wanajaribu kutilia nguvu kauli yao katika jambo la haki, nalo ni kutoka kwa ajili ya Jihadi. Na kumbe wao walikuwa na wenzao walio toka kwenda kupokonya mali ya Makureshi yaliyo kuwa yanakwenda Sham, na wasiyapate. Kikundi hichi kikakhiari kurejea baada ya kuona wamenusurika, kwa kujuvywa na Mtume, na kwamba makafiri wanawaogopa, na kwa kuwa hadi wakivichukia vita, na kuwa hawajui litalo wapata. Na walipo kuwa wakiviendea vita walikuwa kama wanao sukumwa kwenda kufa, na wao wanaona kitacho wauwa, na yanawapata mateso yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Likawa linabishana na wewe, ewe Nabii, kundi hilo la Waumini kuhusu kupigana baada ya kuonekana wazi kwamba hilo ni lenye kutokea, wakawa kana kwamba wao wanaongozwa kupelekwa kwenye kifo na hali wakikitazama waziwazi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net