Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 5

Al-Anfaal 8:5

الأنفال

كَمَآ أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِنۢ بَيْتِكَ بِٱلْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ لَكَـٰرِهُونَ

Maana

Kama alivyokutoa Mola wako Mlezi katika nyumba yako kwa haki, na hakika kundi moja katika Waumini linachukia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kama Mola wako Mlezi alivyo kutoa nyumbani kwako kwa Haki, na hakika kundi moja la Waumini linachukia. [5]

[5] Ushindi, bila ya shaka, upo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Na funguo za mambo yote ziko kwake. Na hali ya Waumini katika kukhitalifiana kwao katika mambo ya ngawira ni kama hali yao pale alipo kuamrisha Mwenyezi Mungu utoke ukapigane na washirikina katika Badri, nayo ni Haki iliyo thibiti. Kwani miongoni mwa Waumini kulikuwapo na kikundi kilicho chukia vita kweli kweli.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama mlivyotafautiana juu ya ugawaji wa ngawira, na Allah Mtukufu Akauondoa kwenu na Akauweka kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake, sala na salamu zimuendee, hivyo ndivyo Mola wako Alivyokuamrisha utoke Madina uende kupambana na msafara wa Makureshi kwa wahyi aliyokujia nao Jibrili, pamoja na kuwa kundi miongoni mwa Waumini walichukia kutoka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net