Al-Anfaal 8:4
الأنفالأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُمْ دَرَجَـٰتٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ
Hao ndio Waumini wa uhakika. Wana vyeo kwa Mola wao Mlezi, na kusitiriwa dhambi, na riziki tukufu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi. [4]
[4] Hakika hawa wanao sifika kwa sifa hizi ndio khasa wanao sifika kwa Imani kwa haki na kweli. Na malipo yao ni kupata vyeo vya ngazi ya juu kwa Mwenyezi Mungu. Yeye Allah Subhanahu ndiye ataye wapa radhi zake, na maghafira wanapo teleza, na duniani atawapa riziki njema, na Akhera neema ya daima.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa wanaofanya matendo haya ndio wenye kuyaamini kikweli, nje na ndani, yale Aliyowateremshia Allah Mtukufu, watakuwa na daraja za juu mbele ya Allah Mtukufu, msamaha wa dhambi zao na riziki nzuri ambayo ni Pepo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net