Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 3

Al-Anfaal 8:3

الأنفال

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ يُنفِقُونَ

Maana

Wale wanaosimamisha Swala, na wanatoa katika vile tunavyowaruzuku.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ambao wanashika Swala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku. [3]

[3] Na hao Waumini walio wa kweli katika Imani, wanashika Swala kwa kutimiza nguzo zake, na kukamilisha unyenyekevu na ut'iifu, ili wawe daima katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na wanatoa katika mali aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la, kwa ajili ya Jihadi, na mambo yote ya kheri, na kuwasaidia wanyonge.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao wanaendelea kutekeleza Swala zilizofaradhiwa kwa nyakati zake, na katika kile tulichowaruzuku wanatoa kwenye yale tuliyowaamrisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net