Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 2

Al-Anfaal 8:2

الأنفال

إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتُهُۥ زَادَتْهُمْ إِيمَـٰنًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

Maana

Hakika Waumini ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu, nyoyo zao zinaingia hofu. Na wanaposomewa Aya zake, zinawazidishia Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi. [2]

[2] Ama hakika Waumini wa haki na kweli daima wanakuwa na khofu na ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu. Akitajwa Allah Subhanahu, Mwenyezi Mungu Aliye takasika, nyoyo zao hufazaika, na zikajaa khofu. Kwa hivyo kila wakisomewa Aya za Qur'ani Imani yao inazidi kuwa imara, na wao huzidi unyenyekevu na ujuzi, na wala hawamtegemei yeyote ila Mwenyezi Mungu aliye waumba, na ndiye anaye walinda na kuwaendeleza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wenye kumuamini Allah Mtukufu kikweli ni wale ambao akitajwa Allah Mtukufu nyoyo zao zinaingiwa na kicho, wasomewapo aya za Allah Mtukufu zinawazidishia Imani pamoja na Imani waliyo nayo kwa kuyazingatia maana yake na kwa Mola wao wanategemea: hawamtaraji isipokuwa Yeye na hawamuogopi isipokuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net