Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 7

Al-Anfaal 8:7

الأنفال

وَإِذْ يَعِدُكُمُ ٱللَّهُ إِحْدَى ٱلطَّآئِفَتَيْنِ أَنَّهَا لَكُمْ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيْرَ ذَاتِ ٱلشَّوْكَةِ تَكُونُ لَكُمْ وَيُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُحِقَّ ٱلْحَقَّ بِكَلِمَـٰتِهِۦ وَيَقْطَعَ دَابِرَ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Na Mwenyezi Mungu alipowaahidi moja ya vikundi vile viwili kuwa ni chenu. Nanyi mkapenda kwamba kile kisichokuwa kikali ndicho kiwe chenu. Naye Mwenyezi Mungu anataka ahakikishe haki kwa maneno yake, na aikate mizizi ya makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu alipo kuahidini kuwa moja katika makundi mawili ni lenu. Nanyi mkapenda lisilo na nguvu ndio liwe lenu; na Mwenyezi Mungu anapenda ahakikishe Haki kwa maneno yake, na aikate mizizi ya makafiri. [7]

[7] Enyi Waumini! Kumbukeni ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenu kwamba atakupeni ushindi juu ya moja katika makundi mawili, hilo lenye silaha na nguvu. Na hali nyinyi mnapendelea kupambana na hilo kundi jengine lenye mali na watu tu. Na hilo ni msafara wa Abu Sufyan. Nanyi mkakhiari mali yasiyo kuwa na wapiganaji. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu anataka kuithibitisha Haki kwa mapendo yake na uwezo wake na kwa maneno yake yaliyo kwisha tangazwa, na ili aung'oe kabisa ukafiri katika Bara Arabu kwa ushindi wa Waumini. Aya hizi tukufu zinatoa sura ya yanayo pita katika nafsi wakati wa vita, nako ni kutamani kukutana na maadui wachache na kuchukia kukutana na wengi, na kupenda kuteka mali na ngawira; na ilhali Mwenyezi Mungu Mtukufu anataka kuitukuza Dini na ishinde Haki na wang'oke makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbukeni, enyi wenye kujadili, ahadi ya Allah Mtukufu kwenu kuwa mtapata ushindi juu ya moja ya mapote mawili: msafara na bidhaa unazozibeba au jeshi la maadui, mpigane nalo na mlishinde. Na nyinyi mnapenda kupata ushindi juu ya msafara badala ya kupigana. Na Allah Mtukufu Anataka kuuthibitisha Uislamu na kuukuza kwa kuwaamuru nyinyi kupigana na makafiri na kuwamaliza makafiri kwa kuwaangamiza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net