Al-Muzzammil 73:19
المزملإِنَّ هَـٰذِهِۦ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا
Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika Njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi. [19]
[19] Hakika Aya hizi zinazo taja ahadi ya Mwenyezi Mungu ni mawaidha. Kwa hivyo mwenye kutaka kunafiika kwazo ataishika njia ya kumwendea Mola wake Mlezi kwa kuchamngu na kunyenyekea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika hizi aya ambazo ndani yake kuna kukhofisha na ukemeaji ni mawaidha na mazingatio kwa watu. Basi mwenye kutaka kuwaidhika na kunufaika nazo, na achukue utiifu na uchamungu kuwa ni njia ya kumfikisha kwenye radhi za Mola wake Aliyemuumba na kumlea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net